top of page
Alhidaaya Da'wah
Elimu Ni Nuru Ya Maisha
Uchumba: Ni taarifa rasmi ya Ndoa inayotolewa kwa wazazi, walezi, au wasimamizi wa Binti, kuwa muoaji anahitaji kumuoa binti yao, na wao kutoa muafaka katika hilo.
Sehemu hii ni Muhim sana kabla ya Ndoa, lakini pia inaweza kuwa sababu ya kuharibu safari Nzima ya ndoa endapo haitozingatia mipaka na taratibu za Kisheria, kwani ndio Msingi wa Mwanzo kabisa wa Ndoa.
Na hapa tutaeleza, uchumba usio sahihi, makosa wakati wa uchumba, na uchumba uliozingatia Sheria.
UCHUMBA
UCHUMBA USIO SAHIHI
1- Wazazi au Walezi kutokuwa na Taarifa.
2- Kumchumbia Mwanamke aliyechumbiwa.
3- Kumchumbia Mwanamke aliyeko katika Eda ya Kufiwa Mume au kuachwa kwa Talaka tatu.
4- Kumchumbia Mwanamke ambaye hajapewa talaka ya Moja kwa Moja.
Wazazi kutoa idhini ya Uchumba
Katika zama hizi watu wengi na hasa vijana wamekuwa wakiingia katika Mahusiano ya Haramu kabla ya Ndoa na kuyaita kuwa ni uchumba, pasina Wazazi au walezi wa binti kujua na kuwaidhinisha kisheria, na haya tumeiga kutoka kwa Wasiokuwa Waislamu, na hili ni kosa na ni madhambi yanayoondoa baraka katika Maisha ya mtu hasa katika Ndoa wanayotarajia kuingia.
Idhini ya Wazazi ama walezi ni amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huanza kwanzia katika hatua za Uchumba, ili Wazazi waone kama mtu aliyekuja kuchumbia ni mtu sahihi kwa binti yao au la, na Sheria hii imewekwa ili kufunga Mlango wa Maasi ikiwa watu watakuwa na Mahusiano yasiyozingatia mipaka ya Sheria: Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Waoweni kwa Idhini ya watu wao" [An-Nisaa: 25]
Kwanza tufahamu Ndoa ni nini katika Sheria ya Uislamu?
Ndoa: Ni makubaliano ya kisheria yanayohalalisha kati ya mwanaume na mwanamke kila mmoja kumstarehesha mwenzake.
Hivyo kila makubaliano ya kustareheshana yasiyofuata sheria, hiyo ni Zinaa, au uchafu mwingineo.
Ndoa ni ibada kubwa yenye baraka nyingi endapo mtu ataiendea kwa elimu, na kufuata miongozo aliyoiweka Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini pia inaweza kuwa ni Jahannam, na mateso makubwa katika Maisha ya mtu endapo ataiendea pasina kufuata taratibu na muongozo aliouweka Mwenyezi Mungu.
bottom of page