top of page

Alhidaaya Da'wah
Elimu Ni Nuru Ya Maisha

Kuhusu Sisi

Tovuti hii inamilikiwa na Sheikh: Abuu Ayman Othman Iddy Othman muhitimu wa Chuo Kikuu cha King Khalid University Saudi Arabia, na ni maalum kwa kutoa darsa, machapisho na vitabu alivyoviandaa.

Lengo letu ni kuwafikishia Waislamu na wasiokuwa Waislamu, popote walipo Duniani, elimu sahihi ya Uislamu kwa mujibu wa Qur'an Tukufu, Sunnah Sahihi za Mtume ﷺ, kwa ufahamu wa Salaf Swaleh (Wema Waliotangulia).

DIRA YETU
Kuwa Tovuti bora inayotoa elimu ya Dini kwa Misingi sahihi, kwa lugha fasaha ya Kiswahili.
KAULI MBIU
Elimu Sahihi Ni Nuru Ya Maisha

Walimu Wetu

Mwalimu wetu ni Sheikh Abuu Ayman Othman Iddy Othman. Pia tunaweza kuweka Maudhui au machapisho mengine kutoka kwa wanachuoni wakubwa wa Ahlus Sunna Wal-Jama'ah, tukiwa na lengo la kuielimisha jamii kwa usahihi zaidi.

Sheikh Abuu Ayman Othman

Muanzilishi & MMILIKI Mkuu WA TOVUTI HII

Tunamuomba Allah atupe Ikhlas katika Kauli na Matendo, na aturuzuku sote Mwisho Mwema.

bottom of page